CCM Yashinda Kwa Kishindo Uchaguzi Wa Madiwani Arumeru

CCM Yashinda Kwa Kishindo Uchaguzi Wa Madiwani Arumeru

2
0
SHARE

Chama cha Mapinduzi (CCM).

Chama cha Mapinduzi (CCM), kimeshinda kata nne za Arumeru Mashariki katika uchaguzi mdogo wa Madiwani uliofanyika jana
jumapili.

Kata hizo na matokeo yake ni kama ifuatavyo,

Makiba Samson Laizer (CCM) kura 2,029 na Joyce Martin (Chadema) kura 608. Kata ya Ambuleni, Jasephat Jackson (CCM) kura 2,057 na

Dominick Mollel (Chadema) kura 1,201. Kata ya Leguruki
Andason Sikawa (CCM) kura 3,023 na Daniel Mbise(Chadema) kura 287.

Kata ya Maroroni, Yoha Kaaya (CCM) kura 3,568 na Asanterabi Mbise (Chadema) 1,201.

Aidha,katika kata hizo nne jana Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe aliwataka wagombe wote kupitia chama hicho wajitoe kwenye uchaguzi kufuatia kukamatwa kwa mawakala wake na baadhi ya wapiga kura kutishwa na Jeshi la Polisi.

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY