JPM Amwagia Sifa Lukuki JK, Atoboa Siri Ya Kutobomoa Tanesco

JPM Amwagia Sifa Lukuki JK, Atoboa Siri Ya Kutobomoa Tanesco

2
0
SHARE

Hospitali ya Taaluma na Tiba ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (Muhas), Kampasi ya Mloganzila.

Rais, Dkt. John Pombe Magufuli amesema kuwa hakubomoa jengo la Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) lililopo Ubungo alipokuwa Waziri wa Ujenzi kwa kuwa aliogopa kufukuzwa kazi na aliyekuwa Waziri Mkuu, Mhe. Mizengo Pinda.

Rais Magufuli amefichua sir hiyo jana alipokuwa akizindua Hospitali ya Taaluma na Tiba ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (Muhas), kampasi ya Mloganzila na kudai kuwa Waziri Mkuu Mstaafu wa Awamu ya Nne, Mhe. Mizengo Pinda ambaye pia alihudhuria uzinduzi huo, ndio sababu ya kutobomoa jengo hilo baada ya kuzuiwa.

Hatahivyo, amesema kwa sasa waziri mkuu huyo mstaafu hawezi kumzuia kwakuwa sasa yeye ndiye Rais hakuna wa kumzuia na kuahidi kubomoa jengo hilo, lote ama sehemu kama itakavyotakiwa.

“Nilishatoa maagizo, najua Mizengo Pinda kwenye hili alinipinga wakati ule, lakini najua leo hawezi akanipinga kwa sababu mimi
ndiye Rais.

Wakati ule nilikuwa waziri wake, ndiyo maana nilinyamaza nilijua ninaweza nikafukuzwa, hutakiwi kumpinga mkubwa,” amesema JPM.

“Hilo jengo la Tanesco, narudia kama itakuwa ni kubomoa nusu, no problem (hakuna tatizo); kama ni lote hakuna tatizo, pamoja na jengo la wizara ya maji.

Najua katibu mkuu wa wizara ya maji yupo hapa ananiangalia, wakaanze kulitoa eneo lililopo kwenye
hifadhi ya barabara,” amesisitiza.

Machi 6, 2011 akihutubia wananchi katika mkutano wa hadhara Mjini Chato, Mkoani Kagera, Pinda ambaye alisifia utendaji wa Dkt. Magufuli alimwagiza kusimamisha ubomoaji maeneo kadhaa yaliyokuwa kwenye hifadhi ya barabara likiwemo jengo  laTanescohadi Serikali itakapotoa kauli nyingine kuhusu hilo.

Pinda alikuwa akizungumzia hatua ya Dkt. Magufuli aliyekuwa amewaagiza wananchi waliojenga nyumba ndani ya hifadhi ya barabara kuanza kubomoa nyumba hizo na wasitarajie kulipwa fidia.

Alisema spidi (kasi) ya Magufuli ilikuwa kubwa hivyo alimuagiza kusimamisha ubomoaji huo hadi suala hilo litakapojadiliwa na
Baraza la Mawaziri.

Pinda, alisimamisha ubomoaji huo ili kutoa nafasi kwa Serikali kujipanga upya huku akisema kuwa Serikali inamuamini Magufuli
kuwa kiongozi mwenye uwezo na ndio maana ilimpa nafasi akawabane makandarasi wazembe.

Wakati huohuo, Rais Magufuli amesema kuwa sifa za ujenzi wa Hospitali hiyo zinapaswa kwenda kwa Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete kwaku ndiye aliyefanikisha ujenzi wake.

“Rais Kikwete ndiye chachu ya hospitali hii na mimi alikuwa akinituma na kunipa maelekezo kuanzia utafutaji wa eneo hadi upatikanaji wa miundombinu mingine kama barabara hivyo sifa zote ziende kwa Rais Mstaafu Kikwete,” amesema.

“Kila mtu anapenda sifa lakini kwa hili ni Rais Mstaafu Kikwete ndiye anastahili sifa zote,” amesisitiza Rais Magufuli.

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY