Kauli Ya Kuwa Na Pesa Zaidi Ya Serikali Yamponza Kakobe,TRA Wamfungia Kazi

Kauli Ya Kuwa Na Pesa Zaidi Ya Serikali Yamponza Kakobe,TRA Wamfungia Kazi

1
0
SHARE

Askofu Mkuu wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship, Zachary Kakobe.

Kauli ya kuwa na fedha nyingi kuliko Serikali aliyoitoa Askofu Zachary Kakobe,imezua mapya kufuatia Kamishna wa Mamlaka ya Mapato nchi Tanzania TRA ,Charles Kichere kudai kwamba wanafuatilia ulipaji kodi wake.

Kwa mujibu wa Salaam Kamishna huyo amesema kuwa kutokana na kauli aliyoitoa Askofu Kakobe ya kuwa yeye ana fedha nyingi kuliko serikali itabidi mamlaka hiyo imchunguze ili kubaini kama huwa analipa kodi.

“Sisi watu wa kodi kwakweli tumepokea kauli ya Askofu Kakobe kwa unyenyekevu mkubwa sana kwa sababu sisi watu wa kodi tunapenda watu wenye fedha nyingi ili na sisi tuchukue cha kwetu ,kama mtu anafedha kuliko serikali huku tukijua kuwa serikali yetu inatoa huduma mbalimbali kama kujenga barabara, inatoa elimu bure, inatoa mishahara kwa watumishi wote wa umma, inatoa huduma za afya,ulinzi na usalama wa raia lakini tuaambiwa kuwa serikali hiyo inazidiwa na Askofu Kakobe basi ni jambo jema ,”amesema Kamishna Kichere.

Ameongeza kuwa kama Askofu kakobe ana pesa nyingi kuliko serikali lakini sisi kama TRA hatuna kumbukumbu za historia ya ulipaji kodi wake.

Askofu Kakobe pia anadaiwa kukosoa utendaji wa serikali ya awamu ya na kuwataka viongozi wake wakatubu.

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY