Kijembe Cha Zitto Kwa Mbowe Kufuatia Goli La ‘Mkono’ La Tambwe

Kijembe Cha Zitto Kwa Mbowe Kufuatia Goli La ‘Mkono’ La Tambwe

40
0
SHARE

14-1V 1

Mbunge wa Kigoma Mjini na Kiongozi wa Chama cha ACT­Wazalendo, Zitto Kabwe ametumia akaunti yake ya Twitter kutoa ujumbe wa utani kwa Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe ambaye pia ni Mbunge wa Hai, Freeman Mbowe kuhusiana na goli la Amissi Tambwe alilofunga jana katika mechi ya watani wa jadi linalodaiwa kuwa ni goli la mkono.

Zitto ambaye pia ni mshabiki wa Simba ameandika ujumbe huo baada ya mechi hiyo kuisha ambapo timu hizo zilitoka sare ya goli 1-­1, akimkebehi Mbowe ambaye pia ni mshabiki wa Yanga.

Zitto aliandika maneno yafuatayo, “Mwenyekiti wangu Freeman Aikaeli Mbowe anatambua goli la mkono la Tambwe lakini hamtambui Lipumba.”

sad

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY