Kinana Asema Hakuna Waziri Wa Kumkatalia Jambo

Kinana Asema Hakuna Waziri Wa Kumkatalia Jambo

2
0
SHARE

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana amesema kuwa hakuna waziri mwenye ubavu wa kukataa pale anapoamua kumtuma jambo.

Kinana amesema hayo katika mkutano wa hadhara uliofanyika Kijiji cha Moita Bwawani akimnadi mgombea wa CCM wa Kata ya Moita Wilaya ya Monduli, Prosper Damuni.

Amewataka wananchi katika kata 43 zinazofanya uchaguzi mdogo wa udiwani kuwachaguawagombea wa CCM akisema ndicho chama kinachoongoza dola na ahadi zinazotolewa zinatekelezeka na kuacha kupiga kura kwa ushabiki.

“CCM ndiyo chama kilichoshika dola na kama kuna changamoto sehemu yoyote namwambia waziri anayehusika anafika haraka eneo hilo kusikiliza na kutatua changamoto hiyo, hakuna waziri mwenye ubavu wa kukataa nikimtuma,” amesema Kinana.

Amesema wilaya hiyo inakusanya mapato ya ndani ya Shilingi bilioni 2 kwa mwaka wakati bajeti yao kwa mwaka ni Shilingi bilioni 49 kwa mwaka, fedha ambazo zinatolewa na Serikali Kuu hivyo ni muhimu kuwa na diwani anayetoka chama hicho ili kurahisisha maendeleo ya wananchi.

Mkutano huo ulihudhuriwa na wakuu wa mikoa, Mrisho Gambo wa Arusha na Christopher ole Sendeka wa Njombe ambao waliwataka wananchi kutoyumbishwa na kelele za vyama vingine bali wamchague mgombea wa CCM.

Mgombea udiwani, Damuni amewaomba wananchi kumchagua ili alete maendeleo kwa kuzingatia chama chake ndicho kinachotekeleza ilani ya uchaguzi iliyoshinda mwaka 2015 na kuunda Serikali.

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY