Lowassa Awapa Mbinu Mpya Wanaomuunga Mkono CCM

Lowassa Awapa Mbinu Mpya Wanaomuunga Mkono CCM

20
0
SHARE

Edward Lowassa.V 1

Edward Lowassa. Aliyekuwa Mgombea Urais kupitia tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Edward Lowassa amewataka wale wote waliokuwa wanamuunga mkono lakini wamebaki Chama cha Mapinduzi (CCM) kuendelea kushikamana naye na kumpatia taarifa kwa hatma ya nchi.

Mjumbe huyo Kamati Kuu CHADEMA, amewataka kuendelea kumuunga mkono na wenzake ndani ya CHADEMA.

Lowassa ameyasema hayo katika taarifa yake aliyoitoa akiwa anatimiza mwaka mmoja tangu alipojiengua kutoka CCM na kujiunga na CHADEMA.

Amesema ana furaha sana kutimiza mwaka mmoja tangu atoke CCM na kujiunga CHADEMA na kudai kuwa uamuzi ule haukuwa rahisi lakini kwa ushupavu, ujasiri na mwongozo wa Mungu alifanya uamuzi huo wa kihistoria kwa hatma ya nchi.

“Najivunia uamuzi ule kwani umewafungua macho watanzania walio wengi na kuimarisha demokrasia nchini na tangu nijiunge na CHADEMA nimewakuta viongozi na wanachama walio na moyo wa dhati wa kuliletea maendeleo Taifa lao kwa vitendo,” ameongeza.

Amedai kuwa watanzania bado wanataka mabadiliko, sera na mtu mbadala wa kuongoza mabadiliko hayo na imezidi kuthibitika kuwa hawawezi kuyapata ndani ya CCM isipokuwa ndani ya CHADEMA na UKAWA kwa ujumla.

“Nawahakikishia watanzania na wana UKAWA kwa ujumla kuwa sasa hivi nina ari, nguvu na hamasa kubwa kuliko wakati mwingine wowote ule,” amedai Lowassa.

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY