Magufuli Aahidi Bilioni 10 UDSM

Magufuli Aahidi Bilioni 10 UDSM

14
0
SHARE

V 1

Nkrumah

ABDALLAH MZUI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli amesema atasaidia kupatikanna kwa bilioni 10 kwa ajili ya kuanza ujenzi wa mabweni ya wanafunzi Chuo Kikuu cha Dar es salaam ili kusaidia wanafunzi wengi wanaolazimika kupanga nje ya chuo.

Rais Magufuli ameyasema hayo wakati akiweka jiwe la msingi la ujenzi wa maktaba ya kisasa Chuo Kikuu cha Dar es salaam.

“Uzuri mimi nafahamu ukandarasi vizuri nikitoa ‘advance’  (kianzio) bilioni 10 ujenzi wa mabweni utaanza mara moja tafuteni mkandarasi kazi hiyo ianze katika ardhi ya chuo hiki mimi nitasaidia upatikanaji wa fedha ili tusaidie wanafunzi wengi wanaopata tabu kwa kukosa mabweni,” alisema Rais Magufuli.

Kwa upande wake Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Kikwete amesema kwamba Chuo kinakabiliwa na uchakavu wa miondombinu ikiwa ni pamoja na upungufu mkubwa wa mabweni ambapo wanafunzi wanaolala ndani ya chuo ni asilimia 30 na huku asilimia 70 wakiwa hawajulikani wanakolala.

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY