Makamu Wa Rais Amtembelea Lissu Hospitali

Makamu Wa Rais Amtembelea Lissu Hospitali

1
0
SHARE

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan jana Novemba 28, 2017 alimjulia hali
Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema) Mhe. Tundu Lissu anayepata matibabu katika Hospitali ya Nairobi nchini Kenya.

Mhe. Samia Suluhu Hassan alimfikishia salamu za pole kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John
Pombe Magufuli ambaye amemtakia matibabu mema na kupona haraka ili arejee nyumbani na kuendelea na majukumu yake.

Mhe. Tundu Lissu amemshukuru Mhe. Rais Magufuli na Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kumjulia hali na amewatakia heri katika majukumu yao.

“Msalimu Mhe. Rais mwambie namshukuru sana kwa salamu zake na kunijulia hali” amesema Mhe. Tundu Lissu.
Mhe. Lissu alivamiwa na kupigwa risasi na watu wasiofahamika Septemba 7, mwaka huu Mjin Dodoma.

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY