Manji Achukuliwa Na Gari La Wagonjwa Kutoka Central

Manji Achukuliwa Na Gari La Wagonjwa Kutoka Central

13
0
SHARE

16640658_1383442345053089_6024557385772552086_n

img-20161130-wa0008

Mfanyabiashara Yusuph Manji ameonekana akichukuliwa na gari la wagonjwa ‘ambulance’ kutoka Kituo cha Polisi Kati anaposhikilwa tangu siku ya Alhamisi kwa tuhuma za kujihusisha na biashara au utumiaji wa madawa ya kulevya.

Bado haijafamika hasa nini kimetokea kupelekea Mfanyabiashara huyo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Yanga kuchukuliwa kituoni hapo na gari la wagonjwa.

Ndugu msomaji endelea kufatilia mtandao huu kujua undani wa tukio hili kadiri tutakavyopata habari kutoka mamlaka husika.

Manji ni mmoja wa watu 65 waliotajwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kujihusisha na biashara ya mihadarati na alifika kituoni hapo siku ya Alhamisi pamoja na Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima ambaye aliachiwa.

Hata hivyo, gari lake binafsi na lile la wagonjwa lililombeba yalionekana katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili yakiwa yamesimama katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete.

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY