Mkuchika Ashinda Kesi Ya Ubunge Newala

Mkuchika Ashinda Kesi Ya Ubunge Newala

10
0
SHARE

V 1

ABDALLAH MZUI

Mbunge wa Newala mjini kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) George Mkuchika, ameshinda kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi wa ubunge iliyofunguliwa na aliyekuwa mgombea ubunge wa jimbo hilo kupitia Chama cha Wananchi (CUF) Juma Manguya.

Ushindi huo umetokana na maamuzi ya mahakama kuu kanda ya Mtwara kutupilia mbali kesi hiyo ambayo ilikuwa ikisikilizwa katika mahakama ya wilaya ya Newala, ambapo hukumu iliyosomwa na Jaji Amour Khamis ilisema mlalamikaji ameshindwa kuthibitisha katika kesi yake kwa kiwango stahiki kwamba uchaguzi huo haukuendeshwa kwa mujibu wa sheria.

Akizungumza baada ya hukumu hiyo, wakili wa Manguya, Rainery Songea amesema hajakubaliana na maamuzi hayo na kwamba taratibu zimeanza kufanyika ili kuweza kukata rufaa lakini kwanza atahitaji apate nakala ya hukumu iliyosomwa na Jaji.

Hata hivyo, mahakama hiyo imetoa nafasi ya kukata rufaa kwa mtu yoyote ambaye hatokubaliana na maamuzi yaliyoamriwa.

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY