ORIGI AMKIMBIZA BENTEKE LIVERPOOL

ORIGI AMKIMBIZA BENTEKE LIVERPOOL

28
0
SHARE

Na Zuhura Simba

Subra ya Vuta Heri kwa yoyote mwenye Subra ana fungu lake kwa ahadi iliyowekwa, fungu hilo unaweza ukapata ukiwa Hai au umekufa, mungu ameeleza katika Vitabu. Divork Origi anaoneka kubahatika na Subra yake na sasa ana anza kula ‘Pension’ yake pale Anfield.

AMETOKA WAPI DIVORK OKOTH ORIGI?

Safari yake imeanzia Mbali alitoka Kr Gent ambayo Samatta ana ng’aa nayo kwa sasa baada ya hapo amesajiliwa na Lille ya France,Origi ameonekana zaidi katika mashindano ya Ulaya 2012 akiwa na timu ya Taifa ya Ubelgiji hapo ndipo Brendan Rogers alipo muoma na kumsajili.

SUBRA YAKE NDIO MANUFAA YAKE

Alifanya Subra baada ya kusajiliwa na  na Liverpool alirudishwa kwa mkopo Lille ili aongeze kiwango chake cha kusakata kabumbu baada ya mwaka mmoja akarudishwa Rasmi Liverpool na hakuweza kuanza moja kwa moja alisubiri kwanza ndipo akaanza kupata nafasi.

NAFASI YAKE IKO WAPI SASA?

Baada ya kufanya vizuri kwa mechi tatu mfululizo sasa Mashabiki na Viongozi wa Timu hiyo wanampa nafasi na kuanza kutumainiwa  kuwa katika mipango ya Timu hiyo.

NAFASI YA BENTEKE

Kwa sasa Benteke hana nafasi maana ashapelekwa kuwa chaguo la Nne la timu hiyo Jurgen Klopp  anaonekana hana mpamgo nae na ataweza kuondoka msimu huu endapo ata hitajika kusajiliwa.

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY