RAIS KENYATTA AAPISHWA RASMI.

RAIS KENYATTA AAPISHWA RASMI.

2
0
SHARE

Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta leo ameapishwa rasmi na kuwa Rais wa Taifa hilo linaloongoza kwa uchumi Afrika ya Mashariki
katika utawala wake kwa awamu ya pili.

Kenyatta amekula kiapo mbele ya maelfu ya Wakenya na zaidi ya viongozi 20 kutoka mataifa mbalimbali akiwemo Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, aliyemuwakilisha Rais, Dkt. John Pombe Magufuli na
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema na Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa.

Wakati huohuo polisi wamelazimika kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya wafuasi wa upinzani waliokuwa wamepanga kuendesha ibada ya kuwaombea watu waliofariki katika ghasia za Uchaguzi Mkuu kufuatia wito uliotolewa na Kiongozi wa Upinzani, Raila Odinga aliyewataka wafuasi wake kuwaombea watu waliouawa kwenye ghasia za uchaguzi.

Polisi pia walilazimika kufanya kazi ya ziada ya kuokoa na kupatia baadhi ya wananchi huduma ya kwanza baada ya kuumia pale
walipokuwa wanalazimisha kuingia kwa nguvu katika Uwanja wa Kasarani.

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY