Zitto Kabwe Aitwa Polisi Kuhojiwa

Zitto Kabwe Aitwa Polisi Kuhojiwa

40
0
SHARE

V 1

ABDALLAH MZUI

Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo Zitto Kabwe leo tarehe 7/6/2016  ameitwa Polisi  na Mkuu wa Upelelezi wa Kanda Maalumu ya Dar es salaam  ACP Camilius Wambura.

Kwa mujibu wa Katibu Itikadi, Mawasiliano na Uenezi wa chama hicho  Ado Shaibu, amesema ACP Wambura amemuita Zitto Kabwe kuhojiwa ikiwa ni siku moja imepita tangu azindue operesheni Linda Demokrasia ambayo inatarajiwa kuzunguka nchi nzima kupinga ukandamizwaji wa Demokrasia unaofanywa na utawala wa CCM.

Amesema licha ya Zitto kuitwa na Mkuu wa Upelelezi wa Kanda Maalumu ya Dar es salaam  Wambura ameomba Zitto  asiende leo kwa kuwa ni karibu na masaa ya kufuturu na  kumtaka  aende kesho saa tatu asubuhi.

 Kwa upande mwingine  Shaibu amesema  Chama cha ACT-Wazalendo kitawasiliana na wanasheria wao ili kupata tafsiri ya kimahakama ya uhalali wa jeshi la polisi kuzuia mikutano ya vyama vya siasa ambayo inatambuliwa na kulindwa na katiba.

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY